Mo Beauty's

Mo Beauty's

Share

"Karibu Mo Beauty's – Nywele zako, fahari yako! Hapa ndipo unapopata mitindo ya kisasa ya kusuka, ushauri wa urembo, na huduma zenye ubora

03/05/2026
26/09/2025

✨ Urembo wa Wikiendi ✨
Wikiendi ni muda wa kupumzika, kujifurahisha na pia kung’aa 💄🌹.
Vidokezo rahisi vya kung’aa kabla ya kutoka au hata kukaa nyumbani:

1. Andaa ngozi yako – Osha uso na tumia moisturizer 💧

2. Midomo yenye mvuto – Tumia lip gloss kwa muonekano safi na wa haraka 💋

3. Harufu nzuri – Perfume kidogo huongeza mvuto na kujiamini 🌹

4. Tabasamu na kujiamini – Huo ndiyo urembo bora zaidi 👑

💬 Ni kitu gani huwezi kuacha kufanya ukiwa unaandaa muonekano wako wa wikiendi?

25/09/2025

Mo Beauty’s IMERUDI ✨
"Karibu tena kwenye dunia ya urembo na kujitunza 💄💅🏽
Welcome back to Mo Beauty’s – your home for beauty tips, advice, and self-love inspo. 💕
Stay tuned / Endelea kutufuatilia kwa content mpya kila wiki!"

25/07/2025

🟢✨ MORINGA na ASALI kwa ngozi yako! ✨🍯
Je, unajua kwamba mchanganyiko huu ni silaha ya asili dhidi ya matatizo ya ngozi?

📌 Faida za MORINGA kwa ngozi:
🌿 Hujaza virutubisho muhimu k**a Vitamin A, C na E
🌿 Hupambana na uzee wa ngozi (anti-aging)
🌿 Husaidia kuondoa mabaka, chunusi na weusi usoni
🌿 Hutoa mng’ao wa asili na kufanya ngozi iwe laini

📌 Faida za ASALI kwa ngozi:
🍯 Ni natural moisturizer – hufanya ngozi yako kuwa na unyevu muda mrefu
🍯 Inaua bakteria – huzuia na kutibu chunusi
🍯 Huondoa makovu na mabaka madogo
🍯 Inatoa ngozi iliyokufa na kuiacha ngozi mpya ing’ae

🌸 Ukiunganisha MORINGA + ASALI = ngozi yenye afya, uangavu na urembo wa asili!
Ni salama kwa aina zote za ngozi 💚

🧴Njia rahisi ya kutumia nyumbani:
✅ Chukua unga wa moringa kijiko 1
✅ Changanya na asali ya asili kijiko 1
✅ Paka usoni kwa dakika 15 kisha ioshe kwa maji ya uvuguvugu
✅ Fanya mara 2 kwa wiki kwa matokeo ya haraka!

💬 Je, umewahi kutumia moringa kwenye ngozi yako? Iandike kwenye comment 👇
Follow ’s kwa tips zaidi za urembo wa asili! 🌿✨

30/06/2025

🌸 KARIBU MO BEAUTY'S 🌸

Ngozi yako, Urembo wako, Uhalisia wako!

Karibu kwenye ukurasa mpya wa Mo Beauty's – mahali ambapo urembo wa asili unakutana na tiba ya kweli ya ngozi. Hapa utapata:

✨ Dawa za asili za chunusi na mabaka
✨ Masks rahisi unazoweza kutengeneza nyumbani
✨ Ratiba za skincare za kila wiki
✨ Elimu ya ngozi na miili yetu
✨ Ushawishi na motisha kwa wanawake k**a wewe

🎯 Malengo yetu ni moja tu – kukusaidia uupende uso wako kila siku bila kujificha!

👑 Usisahau kulike, kushare na kufuata ukurasa huu kwa ajili ya vidokezo vipya kila wiki!

26/06/2025

👑 Wanawake wa Kisasa, Hii ni Zawadi Yenu! 💋
Unajua kuwa muonekano wako ni sauti yako ya kwanza kabla hujasema chochote?
Katika dunia ya sasa, urembo si anasa tena, ni nguvu.
Na hapa Royal S**a Trands, tunakuletea:

✨ Siri za ngozi ang’avu
💄 Mitindo ya kisasa ya nywele na urembo
🌿 Tiba za asili kwa ngozi na nywele
💅 Mafuta na sabuni bora zinazotengenezwa kwa mikono ya upendo

📌 Tufuate sasa kwa elimu, mitindo, na bidhaa zinazokupendeza – kwa bei nafuu lakini zenye thamani kubwa!
👭 Uko hapa kwa sababu unastahili kupendeza bila kuumia mfuko!

👇 Bonyeza "Follow" kisha tuma DM upate zawadi yako ya kwanza ya bure ya ushauri wa ngozi!
**aTrands

19/06/2025

> "Je, unajua? Maganda ya limao yanaweza kusaidia kuondoa weusi usoni na kupunguza mafuta!
Zisitupe! Saga ukichanganya na asali, paka usoni mara 2 kwa wiki kwa matokeo ya ajabu!
💛 Tujifunze zaidi kila siku!
**aTrands "

💅 Post ya Ushauri kwa Wasichana

> "Kuwa msichana wa tofauti. Mpenda usafi, anayejiheshimu, na anayejiamini.
Vipodozi vinakupa mvuto, lakini tabia njema ndiyo inakufanya uwe wa kipekee.
👑 Endelea kung’aa, malkia!
**aQueens

13/06/2025

🌿✨ IJUMAA YA NGOZI NA NAFSI YENYE UTULIVU ✨🌿
⠀
Ijumaa imefika, mrembo! Ni muda wa kuweka kando msongamano wa wiki na kuipa ngozi yako hewa safi na upendo. Ngozi yako haijahitaji urembo wa gharama, inahitaji muda wako na upendo wako.

✅ Osha uso kwa maji ya uvuguvugu
✅ Tumia rose water au tonika ya asili
✅ Paka mafuta yako unayopenda
✅ Vaa tabasamu la uhakika – hilo ndo glow halisi 😍
⠀
🧖🏽‍♀️ Leo ni siku nzuri ya kujiandalia mask ya nyumbani – unahitaji dakika 15 tu, si zaidi. Ngozi yako itakushukuru!
⠀
💬 Komenti “GLOW FRIDAY” k**a utajitunza leo 💛
⠀
**aTrands

11/06/2025

🥕✨ KAROTI NA UZURI WA NGOZI ✨🥕
⠀
Unajua? Karoti si kwa ajili ya chakula tu – ni hazina ya urembo wa asili! Ngozi yako itakupenda zaidi ukianza kutumia karoti kwenye matunzo yako 😍
⠀
Faida kuu 3 za karoti kwa ngozi ni:
1️⃣ Inasaidia kuondoa chunusi – ina vitamin A ambayo hupambana na bakteria wa ngozi
2️⃣ Hulainisha na kung’arisha ngozi – betacarotene husaidia ngozi kuwa soft na yenye mwangaza
3️⃣ Huondoa makovu na kuboresha rangi ya ngozi – husaidia ngozi kurekebisha seli zilizoathirika

🧴Unaweza kutumia karoti k**a:
– Mask ya uso (karoti iliyosagwa + asali kidogo)
– Mafuta ya karoti kwa kupaka kila usiku
⠀
🧡 Ngozi yako ni zawadi. Ipe upendo, ipe karoti!
⠀
👇 Komenti “KAROTI” k**a unataka recipe ya mask ya karoti kesho!
⠀
**aTrands

Want your business to be the top-listed Beauty Salon in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

Yombo Vituka
Dar Es Salaam
151101

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mo Beauty's posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Dar es Salaam.